Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo, Omar Said Shaaban, ameitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutoa majibu ya kina juu ya hoja tatu zinazoibuka kutokana na uamuzi wake wa kuwaruhusu baadhi ya watu kupiga kura tarehe 27 Oktoba, siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.